CHILA – MODULI CWS

Fomu Ya Uchunguzi

KOMPAKTI NA YENYE NGUVU
Mifumo ya CWS MODULI ya Climma ni suluhisho maalum kwa uyoyozi-hewa kwenye majahazi kutoka futi 60 hadi majahazi makubwa ya mita 50 na zaidi. Mfumo wa kimoduli uliojengwa na umbo la fremu la chuma cha bila doa ikijumuisha kondensa na chemba anuwai kwa saketi za maji chumvi na maji safi inahakikisha kuwa Climma CWSndio suluhisho kompakti zaidi.

INA UFANISI NA INAAMINIKA
Kichakato kidogo zaidi cha kipekee cha Climma, ndani ya boksi dhibiti lilio kati la CWS, kinasimamia na kucheki vigezo vyote muhimu vya mfumo kwa kutumia itifaki ya onyesho la Modbus kuboresha zaidi utenda kazi na kuaminika kwamfumo huu. MODULI CWS zote pia zinapatikana zikiwa na viendeshi vya invata. Invata za kipekee za Climma za kujipoza kwa maji zinaondoa karenti ya kuwasha kabisa na kupunguza matumizi ya nguvu ya vifaa vya CWS kwa hadi 30%.

ILIYOJENGWA KWA UBORA WA KIWANGO CHAJUU ZAIDI
Kondensa ya maji  ya bahari na saketi husika ya maji ya bahari na chemba anuwai zimeundwa na cupronickel ya daraja-marini kwa kuzuia kwa kiwango cha juu zaidi kukorodi kwa maji ya bahari. Saketi ya maji safi imeundwa na shaba na chuma kisicho na doa na kila kigandamizaji kinashikiliwa na viambatinishi dhidi-uvumaji ndani ya kijumba cha fremu cha chuma kisicho na doa. 
Ubunifu wa kimoduli unamaanisha kuwa Climma CWS MODULI inaaminika sana na urudufishaji uliojengwa kwenye muundo. Kila kigandamizaji kinajitegemea kikamili na kinaweza kurukwa kwenye mfumo, ikihitajika; hata inaweza kuondolewa kutoka mahali pake kwa marekebisho, ikiacha mfumo uliobaki ukifanya kazi kikamili na utulivu wa ndani ya chombo ukiendelea kwa kiwango hichohicho au kiwango cha juu zaidi. Kwa usawa, ikihitajika, moduli za ziada zinaweza kuongezwa kwa mfumo uliopo kuzidisha uwezo wa kushukisha joto wa mfumo mzima.
Viunganisho vyote vya kiumeme vimeundwa tayari, vikiwacha baadhi yaviunganisho asili pekee kwa uwekaji wa mwisho. Kila moduli na pia mfumo mzima unapimwa kisahihi kulingana na viwango vya kudhibiti ubora wa kiwango cha juu zaidi.

MAELEZO MAALUM YALIYOLENGWA YANAYOFAA
Inapatikana kutoka 72.000 hadi 576.000 BTU/h ikiwa na uhuru wa kuchagua mzunguko kinyume au poza pekee, ubunifu wa kimoduli unahakikisha kuwa kila mfumo CWS unaboreshwa kulingana na ukubwa haswa wa jahazi na kutoa utoaji BTU/h wa kiwango cha juu zaidi kutoka kwa nafasi ndogo zaidi.
Fremu zinazounganishwa pamoja kuunda rafu kama inavyohitajika na pia inawezekana kubadilisha nafasi ya saketi za maji ya bahari. Fremu zinaweza kupakwa rangi kulingana na vifaa vilivyobaki kwenye chumba cha injini au nafasi ya mashini kuhakikisha kuwa mfumo unaonekana mzuri kama unavyotenda kazi; fremu pia zinaweza kufinikwa na paneli zilizojihami. Mfumo wa CWS MODULI pia unaweza kupangwa bila fremu.

Specifications :

  • Uzito: : 160 - 780 kg
  • Urefu: : 653 - 704 mm
  • Upana: : 810 - 2220 mm
  • Mtindo Baridi: : 21 - 253 kW